MAWAZIRI wa Utalii wa nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC), wanatarajia kukutana mwishoni mwa mwezi huu kujadili
pamoja na mambo mengine, migogoro ya kimaslahi katika sekta ya utalii katika
nchi zao.
Ajenda kubwa
ya mkutano huo itahusu mgogoro kati ya Kenya na Tanzania kuhusu kuzuiliwa kwa
magari ya kusafirisha watalii kuingia na kutoka katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta, jijini Nairobi.
Akizungumza
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Kupinga Ujangili, Waziri wa
Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Lazaro Nyalandu,
amesema kuwa, wanatarajia kukutana Machi 20 jijini Arusha na kueleza kwamba,
tofauti hizo zitajadiliwa na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu. Waziri Nyalandu
amesema kuwa, Tanzania haitakubali kupoteza maslahi ya Watanzania na taifa kwa
ujumla. Amesema kama ninavyomnukuu: "kilichotokea awali kwa sasa hakiko
tena, mahusiano yetu na Jamhuri ya Kenya ni mazuri, kwa sababu hiyo tumeafikiana
na mawaziri wa nchi hizo kukutana ili kuangalia njia ya kumaliza mvutano
unaoshindaniwa katika eneo hilo. Mwisho wa kunukuu. Ikumbukwe kuwa, Desemba
mwaka jana, serikali ya Kenya ilizuia magari yote ya Tanzania yanayosafirisha
watalii kutoka na kuingia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta,
hali ambayo imezua mikwaruzano kati ya Kenya
No comments:
Post a Comment