Wafanyabiashara nchini Burundi |
SHIRIKA la kiraia
la kupambana na ufisadi na ughali wa bidhaa nchini Burundi limetishia kuitisha
mgomo wa nchi nzima nchini humo.
Shirika hilo limemtishia Rais Pierre Nkurunziza kwamba, siku
ya Alkhamisi litaitisha mgomo wa nchi nzima. Taarifa ya shirika hilo la kiraia
imebainisha kwamba, litasubiri jibu la Rais Nkurunziza hadi hatua ya mwisho
kabla ya kuitisha mgomo huo.
Uamuzi wa shirika hilo la kiraia umetokana na kuongezeka bei
za bidhaa muhimu kama mafuta, kupanda kwa kodi za simu na mengineyo.
Serikali ya Burundi imenukuliwa ikitangaza juu ya kuweko
juhudi za baraza la mawaziri la kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo. Shirika la
Kupambana na Ufisadi la Ughali wa Bidhaa nchini Burundi limeshamtumia barua
mbili Rais Pieere Nkurunziza wa nchi hiyo likielezea wasi wasi wake kuhusiana
na kuchelewa kutolewa majibu ya matakwa yao. Mkuu wa shirika hilo, Gabriel
Rufyiri amesema kuwa, wamebainisha wazi kuhusiana na tatizo hilo na wanasubiri
majibu kwa kiwango hicho hicho cha uwazi. Amesema, endapo serikali ya Rais
Nkurunziza itashindwa kutoa majibu ya kueleweka hadi kumalizika muda walioutoa,
basi watawataka wananchi wa Burundi wafanye mgomo wa siku nzima siku ya
Al-Khamisi.
No comments:
Post a Comment