Dkt Kiza Besigye |
Kiongozi wa chama hicho, Dkt Kizza Besigye, ambaye amekuwa
akiwania urais amekuwemo ndani ya ofisi hizo na wanahabari waliokuwa katika
eneo hilo wanasema polisi wameondoka naye akiwa kwenye gari lao.
Kituo cha televisheni cha NBS kimeripoti kuwa Besigye na rais wa
FDC Mugisha Muntu wamekamatwa katika makao makuu hayo eneo la Najjanankumbi, na
wafuasi wa chama hicho wakatawanywa kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi.
Mke wa Dkt Kizza Besigye, Winnie Byanyima, ameandika kwenye
Twitter kwamba kiongozi huyo wa upinzani bado anazuiliwa katika kituo cha
polisi cha Nagalama pamoja na Jenerali Muntu. Askari anayewalinda anasema amewapa
mkeka wa kulalia.
No comments:
Post a Comment