Monday, July 7, 2014

WANANCHI wamiminika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam


Viwanja vya sabasaba Kilwa Road jijini Dar es salaam

MAONESHO ya 38 ya sabasaba yanaendelea katika viwanja vya  mwalimu Julius Nyerere Barabaraya Kilwa jijini Dar es salaam ambapo viongozi na wananchi mbalimbali wanajitokeza kuangalia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na makampuni ya ndani na nje ya nchi.

Leo ni tarehe saba ambayo yanaashiriwa uasisi wa sikukuu hiyo ambapo awali ilikuwa ni ya wakulima lakini kutokana na mabadiliko ya kisera wakulima watakuwa wakisheherekea sikukuu ya tarehe nane  mwezi wa nane maarufu kama nanenane.
Kauli mbiu ya maonesho ya sabasaba ya mwaka huu ni kuunganisha uzalishaji na masoko.

No comments:

Post a Comment