Monday, February 29, 2016

WAKULIMA 400 wilayani Kilombero hatarini kukumbwa na njaa

ZAIDI ya wakulima  400 wa mpunga katika kijiji cha Mkangawalo wilayani Kilombero wamesema kuwa wapo hatarini kupata baa la njaa baada ya hekari zao 1000 za Mashamba ya mpunga kukauka kwa madai ya kampuni ya Kilombero Plantation Ltd (KPL)kunyunyuzia dawa ya kuua magugu kwa kutumia ndege na kuingia katika mazao yao.

 Wakizungumza na waandishi Wa habari,wananchi hao wamedai kuwa licha ya kuzuiwa kutumia ndege kunyunyuzia dawa katika Mashamba yake lakini mwekezaji Huyo amekuwa mkaidi na kuendelea na zoezi hilo ambapo alifanya zoezi hilo mara mbili kati ya Januari 26 na Februari 12 mwaka huu.
 Wakielezea wanavyoathirika wakulima hao wamesema kuwa wakati kampuni hiyo ikiandaa mashamba kwa kunyunyuzia dawa katika Mashamba yake kwa kutumia ndege upepo usababisha dawa kuingia katika Mashamba ya wakulima na kuua mazao yao kwani wakulima uanza kupanda mazao kabla ya mwekezaji huyo.

"Hali iliyopo katika mashamba yetu ni mbaya baada ya mazao kukauka huku pia hali hii inatishia Afya zetu tokana na dawa kuingia hadi kwenye Maji ya visima tunavyotumia sisi na Mifugo na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na Wilaya juu ya mwekezaji huyo," alisema Renatus Mtemele.

Naye Benadicta Ng'ongola alisema kuwa mwekezaji Hugo amekuja kuangamiza wananchi Wa Mkangawalo kwani mwaka 2010 alizuiwa kutumiwa ndege kumwagia dawa katika Mashamba yake na kweli alisimama toka mwaka huo hadi sasa baada ya kuua mazao ya wakulima na kulipa fidia ya shilingi milioni 50,lakini wanashangaa mwaka huu amerudia tena zoezi hilo na kuathiri tena Mashamba ya wakulima.


"Toka mwaka 2010 alipopigwa marufuku alikuwa anatumia matrekta katika umwagiliaji na hakukuwa na madhara katika Mashamba yetu ila mwaka huu amerudia zoezi la kutumia ndege na madhara yameonekana hivyo tunaiomba serikali kutusaidia lasivyo tutavuna mpunga wake 

No comments:

Post a Comment