Manispaa ya Morogoro |
Hayo yamebainishwa
karibuni kwenye baraza la madiwani na Meya wa manispaa hiyo Paschal Kihanga
akifafanua kuwa kati ya kisi hicho cha fedha shilingi Bil.7.5 zilizokopwa benki
ya CRDB zitatumika kujenga vitegauchumi likiwemo jengo la kisasa maarufu DDC na
soko kuu la kisasa.
“fedha hizo shilingi
Bil.7.5 ni asilimia 75 ya gharama ya mradi manispaa inataraji kuchangi asilimi
25 na tayari upembuzi yakinifu wa ujenzi wa soko kuu la kisasa
umefanyika”alisema Kihanga.
Aidha alisema ndani ya
shilingi hizo Bil.8.774, shilingi Mil.927 zinataraji kujengea kilomita 2.46 za
lami mjini humo ikiwemo barabara ya Regasore, Mtoni na Mdaraka sambamba na
kuweka tabaka jipya la lami katika barabara ya Uhuruna Nkomo zenye urefue wa
kilomita 1.28.
“shilingi Mil.250
tunatarji kutengenezea kilomita 4 za mifereji ya maji ya mvua eneo la Ipo
ipo-Kihonda magorofani na barabara ya kichangani huku shilingi Mil.97 tumepanga
kuboresha maeneo korofi barabara ya
Chamwino,Mkundi-Kinglwira,Misongeni-Kinglwira,Lukuyu na Area Five”Aliongeza
meya huyo.
Mbali na fedha hizo
kutengwa kwa ajili ya miundombinu,Meya huyo alisema Manspaa hiyo inalenga kuondoa
vifo vya watoto na mama wajawazito kwa kupeleka ombi maalumu la shilingi
Bil.2.5 kutoka Tamisemi ili kukamilisha ujeni wa hospitali ya manispaa ambayo
tayari imeanza kujengwa.
No comments:
Post a Comment