NCHINI Zimbabwe watu milioni tatu wanakabiliwa na baa la njaa
kufuatia ukame uliosababisha mifugo elfu 20,000 kufa.
.Akiongea wakati wa sherehe za siku yake
ya kuzaliwa, rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, alikiri kuwa taifa hilo linakabiliwa
na madhara ya uhaba wa mvua kutokana na hali ya hewa ya El nino.
Zimbabwe inakabiliwa na hali kali zaidi
ya kiangazi kuwai kushuhudiwa kwa kipindi cha miongo mitatu.
Kwa sasa, robo
ya raia wa taifa hilo wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
Maelfu ya
wanyama pia wameangamia.
Rais Robert
Mugabe tayari ametangaza hali hiyo kuwa janga la kitaifa, na hivyo inafungua
njia kwa wafadhili kuingilia kati.
Tsvanginde
Mutandavari anaishi katikia kijiji cha Tsvimborume , kilomota 400 kutoka
Harare.
Anawategemea
wanawe wawili wanaoishi Afrika Kusini kwa chakula, japo huwa nadra sana kwa
wanawe kumtumia pesa.
No comments:
Post a Comment