Wednesday, March 4, 2015

MBUNGE wa Morogoro mjini akabidhi matundu kumi ya choo


Mbunge wa Morogoro Mjini Abdul Aziz Abood(kati)
HATIMAE mbunge wa Morogoro mjini AbdulAzizi Abood amekabidhi matundu 10 ya vyoo vya kisasa yaliyogharimu shingi 7,500,000 yakiwemo mawili ya walimu katika shule ya msingi Mkwajuni kata ya Kichangani pia kukagua ukarabati wa barabara za lami unaoendelea mjini humo kwa gharama ya shilingi Mil.536.5.


Kujengwa na kukabidhiwa kwa matundu hayo kati ya 24 yanayohitajika shuleni hapo kunatokana na uzembe wa uongozi wa kata na shule hiyo kuliosababisa kukosa vyoo kwa wanafunzi na walimu kwa muda mrefu hivyo wakaguzi wa shule kutishia kuifunga.

Akikabidhi matundu hayo kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo Theresia Mahongo, mbunge Abood alisema ameamua kuinusuru shule na kifungo hicho akitumia fedha zake za mfukoni ili kuwaepusha wazazi na kero ya kufukuzana na migambo wa manispaa kusaka michango bila kujali ukata unaowakabili.

Awali kabla ya makabidhiano hayo kuliibuka malumbano ya kisiasa bada ya mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na mendeleo Chadema katani humo Abdalah Kumburu kumshukuru mbunge huyo kwa kurejesha fedha za mfuko wa jimbo kwa wanachi hao kupitia ujenzi huo. 

"nimpongeze mbunge wetu kwa uwajibikaji wake na moyo wake wa dhati kutumia fedha za mfuko wa jimbo kuokoa janazi la shule kufungwa tunataka wabunge wa namana hii na yeye tunamsihi aendelee hivyohivyo"alisema Kumburu.

Kauli hiyo ilimlazimu Abood kusimama na kusema" jamani tuache malumbano yasiyo na hoja ili kupotosha wanachi,fedha zilizotumika ni kutoka mfukoni mwangu na kama hamuamini njooni ofisini niwaonyeshe mapato na matumizi ya fedha za jimbo"

Kwa upande wake mkaguzi wa shule aliyetaka kuifunga shule hiyo Mwalimu Victoria Bengesi alisema waliamua shule ifungwe baada kujiridhisha kuwa mazingira ya wanafunzi na walimu kufundishia,kusoma na kujifunzia hayakuwa mazuri.

No comments:

Post a Comment