Afisa manunuzi wa H/W Kilombero Dinawi Gabriel akipewa funguo ya Greda |
HALMASHAURI
ya wilaya ya Kilombero imenunua
greda jipya kwa shilingi mil.493 ili kukabili tatizo la ubovu wa barabara zake
sambamba na kukuza uchumi wake kwa kulikodisha.
Katika makabidhiano ya greda hilo
kwa niaba ya mkurugezi Mtendaji wa halmashauri hiyo,Afisa manunuzi wa
halmashauri hiyo Dinawi Gabriel alisema kufika kwa greda hiyo kutaongeza mapato
ya ndani ya halmashauri na pia kupunguza gharama za halmashauri.
Dinawi alisema ununuzi wa greda hilo
ni utekelezaji wa maagizo ya baraza la madiwani la halmashauri hiyo ambayo
waliagiza kununuliwa greda kwa ajili ya kuchonga barabara za halmashauri
sambamba na Roller kwa ajili ya kushindilia barabara hizo.
Alisema kwa sasa wamepata greda na
mwishoni mwa mwezi huu wanategemea kupokea Roller na wametenga shilingi milioni
230 kwa ajili ya ununuzi wa kifaa hicho pamoja na gharama za usajili na
usafirishaji.
Afisa huyo wa manunuzi alisema kuwa
greda hilo limefika wakati muafaka kwani wakandarasi wengi wanaopewa kazi
katika wilaya hiyo wanakosa vifaa vya ujenzi ikiwemo greda na kwa sasa
itarahisisha utendaji wao wa kazi kwa kulilodi greda hilo.
Akielezea utaratibu wa kutengeneza
barabara za vijiji,Dinawi alisema wahusika watatoa gharama ndogo za utendaji
ikiwemo mafuta na malipo kwa opereta huku pia wanaruhusu wilaya jirani
kukodisha greda hilo.
Hata hivyo Dinawi alisema kwa
kipindi kilichopita cha bajeti halmashauri ilipata kiasi cha shilingi bilioni 3
kwa ajili ya matengenezo ya barabara kutoka kwa wafadhili mbalimbali na
shughuli zinaendelea ila wangekuwa na greda lao mapema gharama hizo
zingepungua.
Kwa upande wake Mhandisi mauzo wa
kampuni ya GF Trucks&Equipment Ltd ambao ndio walipewa tenda ya ununuzi
Juma Hamsini alisema greda walilolileta ni aina ya Terex lililotengenezwa
nchini Marekani.
Hamsini alisema wameamua kutoa kwa
mkopo greda hilo kwa halmashauri hiyo tokana na halmashauri hiyo kuwa moja kati
ya halmashauri zinazokuwa kwa kasi na ukuaji huo wa kasi unahitaji huduma za
kijamii na miundombinu.
Mhandisi huyo alisema kampuni
yao ni ya wazawa na inahusika na uuzaji wa mitambo ya ujenzi na
majengo na wanatoa mikopo yenye masharti nafuu na haina riba kwa taasisi za
serikali kwa miezi 12 na wamekwisha saidia zaidi ya halmashauri 60 toka mwaka
2007 na taasisi za serikali 10 kwa kukopesha magari na mitambo.
Alisema katika kuthibitisha kiwango
cha ubora wanatoa garantii ya masaa 2000 au miaka 2 kwa mitambo na kilomita
20,000 au mwaka mmoja kwa magarimagari hivyo kutoa wito kwa watendaji kuwa
mitambo wanayonunua isiwanufaishe wao bali itumike kwa kunufaisha halmashauri
kwa kukodisha wadau mbalimbali
No comments:
Post a Comment