Msitu wa Hifadhi |
Mhariri mkuu wa Mbiu ya
Maendeleo Media Group, Bi
Salma Mlamila ameeleza kuwa kipindi cha Dira ya Mazingira sasa kinarushwa hewani kupitia Redio Jamii ya Kilosa, mkoani Morogoro.
Kipindi hicho kimeanza kurushwa rasmi februari 16, mwaka huu katika
kituo cha Radio Jamiii kinachomilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Kilosa,
mkoani Morogoro.
Kwa takribani miezi mitatu kipindi
hicho kitagusa sekta ya Misitu na kitakuwa kikizungumzia jitihada za wakala wa
Huduma za misitu nchini(TFS), hususani wilayani Kilosa katika kutunza, kusimamia na kuhifadhi misitu
.
Kipindi hicho kitakuwa kikirushwa
kila siku ya jumamosi saa tatu usiku.
Bi Salma Mlamila amewataka wadau
mbalimbali wa mazingira kukiunga mkono kipindi hicho kwa kushiriki kipindi hicho, ambacho kitakuwa kikirushwa
kila siku ya jumamosi saa tatu usiku.
.
Amefafanua kuwa, makala za vipindi hivyo zitakuwa
zikipatikana katika blog ya Mbiu ya Maendeleo ambayo ni
www.mbiuyamaendeleo.blogspot.com
hongera sana Mr Issa Msekwa kwa juhudi zako.ALLAH akupe Tawfiiq
ReplyDelete