Mohamed Morsi |
WAENDESHA mashtaka wa kijeshi wa Misri wamewarejesha Rais wa nchi hiyo
aliyepinduliwa na jeshi Mohamed Morsi na wanachama wa Harakati ya Ikhwanul
Muslimin wanaokaribia 200 katika mahakama ya kijeshi ili kujibu tuhuma
zinazowakabili za kuchochea mauaji.
Mmoja wa waendesha mashtaka ya Misri ameeleza kuwa, kesi mpya
itafunguliwa tarehe 23 mwezi huu.
Kesi hiyo inahusiana na maandamano ya fujo
yaliyotokea katika mji wa Mfereji wa Suez Agosti 14 mwaka juzi, kufuatia
kuondolewa madarakani Rais halali wa Misri Mohamed Morsi, ambaye anatuhumiwa
kuwa alichochea maandamanao hayo ya Wamisri yaliyosababisha watu 31 kupoteza
maisha.
Shirika la habari la Misri MENA limeripoti
kuwa, wanachama 198 wa Ikhwanul Muslimin pamoja na kiongozi wa kundi hilo
Mohamed Badie pia watapaswa kujibu tuhuma zinazowakabili mbele ya jaji wa
kijeshi. Ni vyema kuashiria hapa kuwa, mahakama za kijeshi za Misri ni maarufu
kwa utoaji adhabu kali.
No comments:
Post a Comment