Waziri wa Ardhi akiwa na ujumbe wake pamoja na watendaji wa bodi ya nyumba nchini Sngapore |
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Makazi WilliamVangimembe Lukuvi na ujumbe
wake jana uliwasili nchini Singapore kwa
Ziara ya kujifunza.
Lengo la ziara hiyo ni kwenda
kujifunza namna Serikali ya Singapore
inavyoratibu upatikanaji wa nyumba kwa wananchi.
Waziri Lukuvi akiwa na ujumbe wake walitembelea
Bodi ya Maendeleo ya Nyumba ya Singapore ambayo ina mamlaka ya juu ya uratibu
wa masuala ya nyumba.
Bodi hiyo ya nchini Singapore imeshajenga
jumla ya nyumba laki tisa mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment