Saturday, February 6, 2016

MKUTANO wa kijiji wavunjika , kisa upotevu wa fedha

UPOTEVU wa zaidi ya shilingi Mil.15.9 kati ya Mil 20 zilizokusanywa kwa miezi sita iliyopita katika kijiji cha Kihangaiko kata ya Msata wilayani Bagamoyo umeibua taflani na kusababisha mkutano maalumu wa kijiji hicho kuvunjika baada ya uongozi kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kwa wananchi.

Kuvunjika kwa mkutano huo uliohudhuliwa na kuungwa mkono na Afisa maendeleo wa Kata Deogratus Shayo na polisi kulitokana na wanakijiji kutoridhishwa taarifa iliyosomwa katibu wa fedha kijijini hapo Shani Ally aliyesema kati ya shilingi Mil.20 zilizokusanywa na kijiji shilingi Mil.15 zimetumika kwenye posho za vikao vya wajumbe wa serikali ya kijiji.

katika kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi wa nane 2015,kijiji kilikusanya kutoka kwenye vyanzo vyake vya mapato zaid ya shilingi Mil.20, tayari shilingi Mil.15 zimetumika kulipa posho za wajumbea wa serikali ya kijiji”alisema Shani na kusababisha mlipuko wa kelele za wanakijiji wakipinga.

Hata hivyo juhudi za mwenyekiti wa kijiji hicho Eliazari Kuroli kujaribu kuwatuliza na kumwomba Shani aendelee kusoma taarifa hiyo,uliibuliwa wizi mwingine wa makusanyo hewa ya zaidi ya shilingi 890,000 walizodaia kutokana na ushuru mbalimbali na tozo.

“ndugu zangu tuelewane kwanza nikweli fedha hizi shilingi mil.15 zimetumika kihalali kulipa posho kwenye vikao vya halamashuri ya kijiji …natangaza rasimi kuahilishwa mkutano”Alisema mwenyekiti Kuroli.
Wanakijiji walikataa na kusema inashangaza uongozi huo kutelekeza matatizo yanayowakabili ikiwemo uhaba wa madawati,vyumba vya madarasa na nyumba za walimu badala ke kuendekeza starehe za vikao na mikutano isiyo natija kwao 




No comments:

Post a Comment