Wananchi kijiji cha Tawa, Morogoro vijijini wakiangalia mpira |
MICHUANO ya kombe
la Mbena wilayani Morogoro imekamilisha awamu ya kwanza kwa kumpata bingwa wa kata ya Tawa
baada ya Tawa Stars kuiralua 2-1 timu ya Chipkizi Stars kutoka kijiji cha
Mfidigo katika fainali iliyofanyika katika uwanja wa Tawa.
Michuano hiyo inayofanyika kwa Kata lengo likiwa kupata timu
itakayoshiriki ligi kuu nchini kwa mujibu wa ahadi ya mbunge wa jimbo la
Morogoro Mashariki Prosper Mbena ilijumuisha timu nane katika kata hiyo.
Mabao ya Tawa yaliyoiwezesha timu kupata seti ya jezi na Mpira
yalipatikana dakika ya 32 na 40 wafungaji wakiwa Emanuel Bisi na George Evarist
wakati Chipukizi iliyoambulia seti ya jezi pekee ilitolewa kimasomaso na
Tanziru Mpando dakika ya 82.
“nimeamua kuanzisha michuano ya Kata kwanza tupate wachezaji
mahili tutakaounda nao timu itakayoweka ushindani na tufanikiwe kuingia ligi
kuu lakini tuwe na timu tishio katika jimbo na baadae wilaya…nimeanza na kata
ya Tawa baadae tutaenda kata nyingine”alifafanua Mbena.
Alisema michuano hiyo itafanyika kwa kupata timu mshindi wa kila
kata baadae kwenda kupata timu mshindi wa jimbo huku mipango ikiendelea kupata
taratibu za timu wilaya itakavyoundwa kwa lengo la kupata timu itakayoshiriki
ligi kuu kabla ya miaka mitano kuisha.
Wilaya morogoro inayokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya
ukosefu wa miundombinu ya michezo kama viwanjakutokana na jiografia yake haijawahi
kuwa na timu katika michuano ya ligi kuu ambayo imekuwa ikifanyika hapa nchini
sambamba na kuwepo kwa ligi hiyo nchini.
No comments:
Post a Comment