Waandamanaji wakiwa na mabago jijini Roma |
WATU kutoka miji mbalimbali nchini Italia
wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo, Roma kupinga mpango wa serikali wa
kutaka kuhalalisha kisheria ndoa za watu wa jinsia moja.
Waandamanaji
hao walikusanyika jana katika moja ya maeneo makuu ya kale la Circus Maximus
mjini Roma wakitaka kufutwa uamuzi wa kuujadili mpango huo wa serikali katika
bunge la nchi hiyo.
Mpango
huo ambao uliwasilishwa bungeni wiki iliyopita na unatazamiwa kupigiwa kura na
bunge mwezi ujao wa Februari umesababisha mpasuko mkubwa ndani ya serikali ya
nchi hiyo.
Mpango
huo unaruhusu watu wa jinsia moja kuwa na mahusiano ya kindoa na kuwa na
mamlaka ya kuasilisha mtoto. S
imone
Pillon, mmoja wa waandaaji wa maandamano hayo amesema:"Tunataka sheria hii
ifutwe kikamilifu bila ya hili wala lile".
Franco
Pantuso, mwenye umri wa 71, ambaye alikuwa mmoja wa waandamanaji
amesema:"Sheria hii inapingana na Mungu na inapingana na Biblia; mimi ni
babu, lazima watoto wetu na wajukuu zetu walindwe".
Itakumbukwa
kuwa wiki iliyopita Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki alitoa angalizo
kali la upinzani wa Kanisa dhidi ya ndoa za watu wa jinsia moja aliposisitiza
kuwa familia ya jadi ni "familia anayoitaka Mungu".../
No comments:
Post a Comment