HALMASHAURI ya Jiji la Arusha inakamilisha mchakato wa kupata Sh bilioni
28 za mkopo kutoka Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kwa ajili ujenzi wa soko
jipya la Kilombero.
Mkurugenzi Mtendaji wa jiji hilo, Juma
Iddameabainisha hayo wakati alipozungumza na waandishi wa habari na kusema
kuwa, miundombinu ya soko hilo kwa sasa imechakaa na imefikia mwisho wa uzuri
wake.
Idd anasema, soko hili halifai kukarabatiwa
lakini kubomolewa na kujengwa soko jipya litakalokuwa na miundombinu bora
kuliko ilivyo sasa.
Aidha anasema wanamalizia uboreshaji wa
miundombinu ya Soko la Shuma lililopo katika kaunti ya Elerai ambalo kuanzia
sasa litakuwa likitumika kushushia bidhaa zote zikiwemo matunda, samaki na
vitunguu, na wafanyabiashara watakuwa wakitumia magari madogo kubeba bidhaa zao
hadi soko la Kilombero.
Mkurugenzi huyo pia anasema, magari yote ya
mizigo ya biashara hayaruhusiwi kushusha wala kupakia mizigo ndani ya soko la
Kilombero na hayo ni baadhi ya maandalizi ya soko jipya.
No comments:
Post a Comment