Kivuko cha Kilombero |
WATU watatu akiwemo
dereva wa gari la benki ya CRDB tawi la Ifakara Dustin Wasira na wawili mtu na
mwane ambao hawa kutambuliwa mapema wanasadikiwa kufa maji na fedha kuzama
mtoni Kilombero baada ya kivuko cha Kilombero II kuzama majini.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kuwa nikweli kunataarifa za watu hao kutopatikana
ingawa hakuana maiti yoyoyte iliyopatikana hadi jioni tunakwenda mitamboni.
Wakizungumza na kwa nyakati kati tofauti baadhi ya mashuhuda wa
tukio hilo Prisca Jelemia na Said Kibaba walisema kivuko hicho
kilizama 27/1/2016 saa 3 usiku wakati kikijaribu kuwavusha watu na magari
kutoka ngambo ya pili Ulanga kwenda ngambo ya Kilombero.
Mashuhuda hao walisema inawezekana kilikuwa na mizigo migi
ikiwemo mizigo ya kawaida,abiria na magari kutokana na kuwa ndio
ilikuwa tripu ya mwisho kusha kwa siku hiyo nakuwa kuwa kutokana na hali hiyo
kikiwa kimebakia .
Akizungumzia hali hiyo Mkuu wa Kivuko hicho Mhandisi Fadhir
Haroub alisema Kivuko kilichozama ni MV Kilombero II na kilikuwa katika safari
ya mwisho kutoka upande wa Ulanga kuelekea Ifakara-Kilombero.
Haroub alisema kilipofika katikati ulitokea upepo mkali na
uliokwenda sambamba na mvua kisha kusababisha kusukuma Kivuko na walijitahidi
kukiokoa lakini ikashindikana na hatimaye kugonga nguzo za daraja muda kisha
kusimama na kuzama.
Alisema katika Kivuko hicho kulikuwamo na magari matatu likiwemo
Lori aina ya Fuso lililobeba Michele na land cruiser 2 moja ya Benki ya Crdb na
lingine la kampuni ya KVTC na bajaj,pikipiki na baiskeli kadhaa ila vyote
vimezama na kutojua idadi ya watu waliofariki katika ajali
Kufuatia maaafa hayo serikali kupitia waziri
wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbalawa imeahidi kuongeza
nguvu ya uokozi ikiwemo kuwashirikisha asikari jeshi ili zoezi lifanyike
haraka.
Waziri Profesa Mbalawa akizunguza na wanachi
wilayani Kilombero,alisema serikali imetenga shilingi milioni
885 kwa ajili ya ukamilishwaji daraja la mto huo mapema iwezekanvyo.
No comments:
Post a Comment