Waziri wa habari, Utamaduni , sanaa na michezo Nape Nnauye |
WAZIRI wa
habari,sanaa na michezo Nape Nauye amewaangukia waandishi wa habari nchini
akiwaomba radhi kwa walichotendewa juzi bungeni na kusisitiza dhamira yake ya
kuendelea kutoa uhuru kwa vyombo vya habari nchini kufanya kazi zao kwa ustadi
akiamini hiyo ni chachu ya maendeleo kwa taifa.
Nape alilazimika kusema hayo kwenye mkutano wa Jukwaa la wahariri
nchini(TEF) unaofanyika mkoani hapa kufuatia kuwepo taarifa kuwa wahariri hao
wanakusudia kutoa tamko na kuwaondoa waandishi wao Mjini dodoma na kuzuia
taarifa za bunge kwenye vyombo vya habari wanavyovisimamia.
"nitasema mambo matatu hasa hili ambalo binafsi sielewi
lilitokeaje pale Bungeni baada ya wenzetu wa upinzani kutoka nje...nitamke kwa
niaba ya serikali nitahakikisha hakuna mwandishi atakae fukuzwa kwenye vikao
vile Bungeni kwani tunatambua umuhimu wao pale"alisema waziri Nauye.
Akiainisha mambo aliyokusudia kuyazungumza yaliyojitokeza katika
uongozi wake Nape alisema mbali na kukoseshwa usingizi na uamuziwa serikali
kufuta gazeti la Mawiyo hivi karibuni,kuibuka mtafaruku bungeni juu ya serikali
kubadili muda wa kurusha bunge kupitia shirika la utangazaji nchini TBC na
waandishi kufukuzwa bado anaumizwa na sheria zilizopo akidai zimepitwa na
wakati.
"nikweli sheria zilizopo zina mapungufu maana kuna sehemu
zinapishana na sera ya habari hata mimi nayaona haya lakini ndio sheria
zinazofanya kazi sasa...mtazamo wangu ni kusaidiana nanyi kuboresha mswaada wa
habari uliopo ili uwe na tija katika utekelezaji"aiongeza Nape.
Kuhusu uamuzi wa serikali kusitisha kurusha moja kwa moja
matangazo ya bunge waziri huyo alitaja baadhi ya sababu kuwa ni hofu ya shirika
hilo kuhufia kufilisika kutokana na gahrama kubwa ya urushaji matangazo huku
tijayake ikiwa ndogo.
Alisema hesabu za awali zinaonyesha kwa mwaka shirika hutumia
zaidi ya shilingi Bil.4.2 fedha ambazo hutokana na fungu la matumizi ya ofisi
nakuwa mbali na gharama hiyo pia serikali imebaini kurushwa moja kwa moja
kunasababisha watumishi kutowajibika wakikalia kutazama bunge pia mabadiriko
metokana na tafiti katika mabunge ya nchi zilizoendelea na
No comments:
Post a Comment