Wednesday, January 27, 2016

CHELSEA yatozwa faini ya paundi 65,000 kwa utovu wa nidhamu

MABINGWA  watetezi wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea na West Brom wametozwa faini kwa utovu wa nidhamu uwanjani katika mechi iliyozongwa na ubishi mwezi uliopita.

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA limeitoza Chelsea faini ya pauni £65,000.
West Brom kwa upande wake imepigwa faiani ya pauni £35,000.
Mshambulizi mbishi wa Chelsea Diego Costa alihusika katika mengi ya makabiliano hayo uwanjani.
Mhispania huyo alishambuliana na kiungo cha kati wa West Brom, Claudio Yacob baada ya kuangushwa.
West Brom walijifurukuta kutoka nyuma na kutoka sare na wenyeji wao Stamford Bridge.


No comments:

Post a Comment