Wednesday, January 27, 2016

TATIZO la kimaadili chanzo cha Rushwa barani Afrika

Uganda na Kenya zimefungana ktk nafasi ya 139 zikiwa na lama 25
TATIZO la kimaadili linaonesha kudorora kwa viongozi   mbalimbali wa nchi    za Afrika na haswa kusini mwa jangwa la Sahara.

Takwimu za hivi punde zaidi zinaonesha kuwa ufisadi umesakama uchumi wa mataifa 40 kati ya 46 Kusini mwa jangwa la Sahara.
Mkurugenzi wa Transparency International (TI) kanda ya kusini mwa jangwa la Sahara Chantal Uwimana, anasema kuwa kuanzia kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola hadi kukithiri kwa mashambulizi ya kigaidi bara la Afrika linazidi kujuta kutokana na kukithiri kwa visa vya ufisadi.
Katika kanda ya Afrika Mashariki, Burundi inaongoza kwa kiwango cha juu zaidi cha Ufisadi ikiorodheshwa katika nafasi ya 150 duniani ikiwa na jumla ya alama 21 pekee.
Uganda na Kenya zimetoshana katika nafasi ya 139 zikiwa na alama 25.
Tanzania ina alama 30 na imeorodheshwa katika nafasi ya 117 duniani.
Rwanda ndio taifa lililoongoza katika kanda hii ya Afrika kwa kupigana na ufisadi.
Rwanda inaalama 54 na imeorodheshwa katika nafasi ya 44 duniani.
Botswana ndio inayoongoza barani Afrika kwa vita dhidi ya ufisadi.
Taifa hilo la kusini mwa Afrika lina jumla ya alama 63.
Cape Verde ni ya pili na alama (55), Seychelles ya tatu na alama (55), Rwanda ni ya nne na alama (54), 5;Mauritius (53)nayo Namibia ikiorosheshwa katika nafasi ya 6 na alama (53).
Somalia ambayo imekuwa bila serikali ya kitaifa tangu mwaka wa 1991 ndio taifa linaloongoza kwa visa vya ufisadi.

No comments:

Post a Comment