SHIRIKA la Chakula na
Kilimo Duniani FAO limetangaza kuwa, taathira za mabadiliko ya hali ya hewa
yanayosababishwa na El Nino zitapelekea eneo la kusini mwa Afrika kukumbwa na
ukame mkubwa , hali itakayopelekea mazao mengi kunyauka .
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika hilo hilo ni kuwa, kutokana na kupungua sana mvua katika
maeneo mengi ya kusini mwa Afrika na kutokuweko mazingira ya kupanda mazao nchi
za eneo hilo, inatabiriwa kuwa, idadi ya watu watakaokosa bidhaa muhimu za
chakula itaongezeka sana katika miezi ijayo.
Ripoti hiyo inasema kuwa, kupungua mno unyeshaji mvua katika nchi
ya Namibia kumeifanya sekta ya kilimo nchini humo kukabiliwa na hali mbaya na
hivyo kupungua mno uzalishaji wa mazao katika nchi hiyo. Aidha kwa mujibu wa
ripoti ya mwishoni mwa mwaka uliopita ya Shirika la Chakula na Kilimo Duniani
FAO ni kuwa, zaidi ya asilimia 42 ya wananchi wa Namibia wanakabailiwa na uhaba
wa chakula.
Nchi nyingine ambayo raia wake wanajongewa na baa la njaa ni
Malawi ambapo takribani raia milioni mbili na laki nane wa nchi hiyo
wanakabiliwa na hatari ya kukumbwa na baa la njaa.
Kadhalika Madagascar na Lesotho nazo zinaelezwa kuwa miongoni mwa
nchi zinazokabiliwa na uhaba wa chakula.
No comments:
Post a Comment