Monday, January 25, 2016

MWANDISHI wa habari za upekuzi nchini Kenya aachiwa huru

MWANDISHI mashuhuri wa habari za upekuzi nchini Kenya, aliyekamatwa juzi na kuzuiliwa na maafisa wa polisi, ameachiliwa huru bila kufunguliwa mashtaka.


Yassin Juma alikuwa amekamatwa na polisi kuhusiana na kuchapishwa kwa picha za shambulio la wapiganaji wa al-Shabab kambi ya majeshi ya Kenya eneo la el-Ade nchini Somalia.
Wakati wa kukamatwa kwake, polisi waliandika kwamba alikamatwa kwa sababu ya "kutumia vibaya kifaa cha mawasiliano”.
Alizuiliwa usiku kabla ya kufikishwa katika mahakama mjini Kiambu, viungani mwa jiji la Nairobi.
Hata hivyo hakufunguliwa mashtaka na badala yake alirejeshwa katika makao makuu ya idara ya uchunguzi wa jinai na kisha akaachiliwa huru.
Al-Shabab walisema kuwa waliwaua zaidi ya wanajeshi 100 wa Kenya wakati wa shambulio hilo la tarehe 15 Januari, lakini hilo halijathibitishwa.


No comments:

Post a Comment