MAAMBUKIZI ya VVU-Ukimwi kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto
yamepungua kwa asilimia Tano nchini kutoka asilimia 20 mwaka 2012 hadi kufikia
asilimia 15 mwaka jana.
Hayo
yamebainishwa na wadau wa mapambano dhidi ya ukimwi na vvu katika
semina iliyofanyika mijini Morogoro
Wataalamu hao wamesema,Matokeo ya
kupungua huko kwa maambukizi yanatokana na mwitikio wa matumizi ya kidonge
chenye mchanganyiko wa dawa tatu zijulikanazo kitaalamu TDF,3TC na EFV
zinazotumika tangu mama mjamzito
anapogundulika kuwa na maambukizi hayo.
Katika risala ya afya mkoa kwenye
uzinduzi wa mpango wa kutokomeza maambukizi hayo unaotekelezwa na asasi ya
Tunajali kwa ushirikiano na Wamarekani kwenye mikoa mitano nchini, Mganga mkuu
mkoa Dk.Godfrey Mtei alisema mbali na mafanikio hayo serikali inakusudia
kushusha zaidi maambukizi hayo hadi chini ya asilimia nne mwakani.
Alisema ili kufikia lengo la
kutokomeza maambukizi hayo serikali na wadau wakeTunajali inayoshikiana na
Deloitte,Cristian social services commission-CSSC na USAID inataraji kutoa
mafunzo kwa wahudumu 60 kuazia mwezi Julai ili kuziba pengo la vituo 219
vilivyobaki.
Kwa mujibu wa Dk.Mtei, mwaka jana
serikali ya mkoa wa Morogoro ikishirikiana na wadau wake ilipima wajawazito.
No comments:
Post a Comment