Thursday, October 15, 2015

WENGER ;Hatuogopi kutumia fedha katika soka la uhamisho

Arsene Wenger
MKUFUNZI wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa klabu hiyo haiogopi kutumia fedha katika soko la uhamisho.

Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 60 aliwahutubia washikadau siku ya alhamisi katika mkutano wa kila mwaka na kukiri kwamba klabu hiyo ilikuwa na mauzo ya pauni milioni 344 na faida ya pauni milioni 24.7,na kwamba haina tatizo kifedha.
Arsenal ilimsajili kipa Petr Cech pekee kutoka kilabu ya Chelsea msimu huu.
''Hatuogopi kununua,ninajua nina sifa hiyo'',alisema Wenger.''Iwapo mchezaji ni mzuri tutatumia fedha''.alisema Wenger.
Wenger alikosolewa na baadhi ya mashabiki kwa kutomsajili mshambuliaji yeyote kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho,licha ya kujua kwamba Danny Wellbeck atauguza jereha hadi krisimasi.











No comments:

Post a Comment