Sunday, November 1, 2015

WAWEKEZAJI washajiishwa kuwekeza katika sekta ya nyuki

Mwanahamisi Mapolu (katikati)akitoa ufafanuzi mbele ya wandishi wa habari 
WAKALA wa Huduma  za Misitu Nchini (TFS),wamewataka wawekezaji wawekeze kwenye sekta  ya ufugaji nyuki  ili kutoa matokeo mazuri katika sekta hiyo.

 Hayo yamezungumzwa na Afisa ufugaji nyuki  mkuu  wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Mwanahamisi Mapolu wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.
 Mapolu amesema kuwa  wawekezaji wajikite zaidi katika usimamiaji wa viwanda  vitakavyozalisha vifaa vya kufugia nyuki,visigina asali na mavazi ya kujikinga  wakati wa kulina asali.
Pia wawekezaji wajikite zaidi katika usimamiaji wa  viwanda vitakavyo zalisha bidhaa zitokanazo na nta kama mishumaa , rangi za viatu, vilainisho pamoja na vipodozi.


Mapolu amesisitiza kuwa  sera ya ufugaji nyuki nchini inahimiza ushirikishwaji wa wananchi katika shughuri za nyuki, uhifadhi mazingira na uzallishaji wa mazao ya nyuki yanayokidhi mahitaji ya soko.
Pia sera ya  Taifa ya  ufugaji nyuki nchini inasema kuwa ili kuhakikisha kuwa kuna mfumo thabiti wa biashara ya mazao ya nyuki, udhibiti wa ubora wa mazao hayo ukaguzi na utaimarishwa. Biashara ya mazao ya nyuki itahimizwa kwa kuimarisha huduma za kuaminika za udhibiti wa ubora  na ukaguzi wa mazao hayo.











No comments:

Post a Comment