Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan |
MUUNGANO
wa Klabu za Waandishi wa Habari Nchini (UTPC), umewataka
waandishi wa habari walioshinda nafasi za uongozi wa kisiasa ukiwemo ubunge na
udiwani katika uchaguzi mkuu wa hivi karibuni, wajitokeze hadharani kuutangazia
umma kuwa sasa wanaachana na kazi za uandishi wa habari.
Kauli hio ilitolewa jana na
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan, alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari mjini Morogoro mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano mkuu wa UTPC na
Rais wake, Kenneth Simbaya.
Mkutano huo wa siku mbili ,
umehusisha pia na uchaguzi mkuu wa viongozi wa UTPC na wajumbe wa Bodi ambao
utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo , na ulikuwa na kaulimbinu ya ‘
Tumia Klabu za Waandishi wa Habari kwa maendeleo ya mkoa wako’.
Hivyo alisema kuwa, sheria
za klabu za waandishi wa habari zilizopo chini ya UTPC hairuhusiwi kwa
mwandishi wa habari kuwa ni kiongozi wa vyama vya siasa, licha ya kila mmoja
kuwa na uhuru wa kushiriki masuala ya siasa .
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
UTPC, katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu, baadhi ya
waandishi wa habari walishiriki kufanya kampeni za siasa kwa wagombea na vyama
vya siasa.
“Tangu mwanzo tulifanya
makosa kwa suala hili halikuwekwa wazi kwa mwandishi wa habari ama chombo cha
habari kijiweke wazi ...mwandishi wa habari hakatazwi kuingia kwenye siasa
isipokuwa akifanya hivyo ni budi ajiondoe kwenye uandishi wa habari, “ alisema
na kuongeza. “
Anatakiwa ajitokeze
hadharani na kutangaza kuwa anajiuzulu kazi hiyo , na hata chombo chenye mrengo
wa kisiasa wa chama fulani kinapaswa kuujulisha umma kuwa kinamuunga mkono
mgombea fulani,” alisisitiza. “
No comments:
Post a Comment