Tuesday, July 15, 2014

WAKAZI wa Mtwara waipongeza serikali


Kiwanda cha saruji

WAKAZI wa Mtwara wameipongeza serikali kwa jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa wawekezaji wanajitokeza kuwekeza mkoani humo katika kile kinachoonesha kukabiliana na changamoto za umaskini  zinazowakabili wakazi wa mkoa huo.

Wakiongea na Mbiu ya maendeleo mapema leo mjini Mtwara baadhi ya wananchi wamesema , wanangojea kwa hamu ujenzi wa kiwanda kikubwa cha saruji kinachotarajiwa kujengwa na mfanyabiashara mkuwa toka nchini Nigeria Alhaj Dangote kwani kitakuwa mkombozi wa matatizo ya uchumi kwa wananchi wa mtwara na mikoa ya jirani.


No comments:

Post a Comment