Dr. Abdirahman Duale Beyle |
WAZIRI wa
Mambo ya Nje wa Somalia, Dr. Abdirahman Duale Beyle amesema kuwa, balozi za
Somalia nje ya nchi zimepunguzwa na kufikia 31 kote ulimwenguni.
Duale amesema
kuwa, balozi hizo zimepungua tangu kulipofungwa balozi tisa za nchi hiyo barani
Afrika, Mashariki ya Kati, Asia na hata Ulaya.
Amesema kuwa,
ofisi hizo za uwakilishi wa kisiasa zilifungwa kwa muda kufuatia kuongezeka
gharama za uendeshaji wake.
Waziri wa Mambo
ya Nje wa Somalia amesema kuwa serikali ya Mogadishu imekwishachunguza sababu
zilizopelekea kufungwa balozi hizo tisa na kubaini kwamba suala hilo
halitaathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya Somalia na nchi husika
zilikofungwa balozi hizo.
Amesisitiza
kuwa, hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na matatizo ya kifedha na si kwa sababu
nyenginezo. Amezitaja nchi hizo kulikofungwa balozi za Somalia kuwa ni pamoja
na Tanzania, Burundi, Syria, Ujerumani, Uingereza, Malaysia, Libya, Rwanda na
Sudan Kusini.
No comments:
Post a Comment