Friday, July 4, 2014

UGANDA yasema haitishwi na vikwazo vya Marekani


Waandamanaji nchini Uganda  wakipinga ndoa ya jinsia moja

KATIBU mkuu wizara ya mambo ya nje wa Uganda, Balozi James Mugume, amesema kuwa Uganda haitishwi na vikwazo ilivyowekewa na Marekani kama hatua ya kupinga sheria yake kali kuhusu mapenzi ya jinsia moja.

Balozi Mugume ameelezea kuwa serikali ya Uganda hata hivyo itafanya mazungumzo na Marekani ili kufafanua hatua waliyochukua
Amesisitiza kuwa wataieleza Marekani sheria hiyo inapinga tabia ambayo sio ya kiafrika na maadili ambayo hayakubaliki katika jamii nyingi za kiafrika.
Serikali imesisitiza kuwa vikwazo hivyo havitakuwa na athari kubwa kwa nchi hiyo na pia imekanusha madai ya mashirika ya kijamii kuwa tayari sheria hiyo imechochea ongezeko la dhuluma dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Vikwazo vyenyewe ni pamoja na kufutilia mbali msaada wa kijeshi, kuwapiga marufuku baadhi ya maafisa wa serikali kusafiri nje na kupiga tanji mali zao.Maandamano kupinga mapenzi ya jinsia moja na kumpongeza Rais Museveni kuwa kupitisha sheria hiyo
Kadhalika msemaji wa serikali Ofwono Opondo amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa wananchi wa Uganda wanafahamu kuwa hawatategemea tena msaada wa nchi za Magharibi
Waziri wa mambo ya nje John Kerry, amefananisha sheria hiyo na sheria za utawala wa zamani wa kinazzi nchini Ujerumani.

No comments:

Post a Comment