SHIRIKA la kiraia la Morogoro paralegal limetoa
Mafunzo ya usaidizi wa kisheria kwa wananchi wapatao 25 wa Wilaya Kilosa,mkoani
Morogoro ambao watasaidia jamii masikini
katika kupata haki zao katika vyombo vya kutolea maamuzi.
Akiongea na waandishi wa habari wilayani
mjini Kilosa mapema leo,Mkurugenzi wa shirika hilo la Morogoro paralegal centre
for women and children , Frola Masoy amesema kuwa lengo la kutoa mafunzo hayo
ni kutoa msaada wa kisheria kwa jamii isiyo na uwezo kifedha na haiwezi kumudu
gharama ya kumtumia wakili wa kumsaidia kupata haki.
Masoy amesema pindi wasaidizi wa
sheria watakapokamilika kupata mafunzo hayo wananchi wa hali ya chini wataweza
kupata haki zao tofauti na sasa wanadhurumiwa kwa kukosa msaada wa kisheria na
pia itasaidia kupunguza kesi Mahakamani.
Kwa upande wao, wananchi wanaopatiwa
mafunzo hayo wamelishukuru shirika hilo kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani ni
mambo yanayotokea katika jamii hivyo wamehaidi kuisaidia jamii kupata haki zao.
No comments:
Post a Comment