SERIKALI imeahidi kuwa itaendelea kutekeleza
majukumu yake katika kuwezesha elimu ya juu nchini kuwa yenye ubora na
viwango vya kimataifa kaaajili maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Hayo yamebainishwa mapema leo na waziri wa elimu
na mafunzo ya ufundi Mheshimiwa Sshukuru Jumanne Kawambwa wakati
akifunga maonesho ya tisa ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na tume ya vyuo vikuu
nchini (TCU)katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Waziri
Kawambwa amesema kuwa, serikali imefungua milango kwa watu na Taasisi binafsi
kufungua vyuo vikuu ili kuharakisha
maendeleo ili nchini na jukumu la
serikali litakuwa kuwapatia msaada wa mikopo kwa wananfunzi wanaojiunga na vyuo
vikuu hivyo.
Katika maonesho
hayo ya vyuo vikuu nchi kumi na moja zimeshiriki mwaka huu ambapo vyuo vikuu
ishirini toka nchini China vimeshiriki.
No comments:
Post a Comment