Friday, May 23, 2014

WIZARA ya mifugo na uvuvi inafanya jitihada mbalimbali kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maafisa ugani wa uvuvi



SERIKALI inakabiliwa na ukosefu wa maafisa ugani mia sita  kukamilisha idadi kamili inayotakiwa ili kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri wa mifugo na Uvuvi Dokta Titas Kimani ameelza hayo bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake.

Amesema idadi kamili ya maafisa ugani wa sekta ya uvuvi wanaotakiwa nchi nzima ni 1500  wakati waliopo kwa sasa ni mia tisa.
 Hata hivyo waziri huyo wa mifugo amesema , jitihada mbalimbali zinafanyika katika kukabiliana na hali hiyo ikiwemo kuongeza udahili wa wanafunzi wa kozi za uvuvi katika vyuo mbalimbali vya uvuvi nchini kwa ngazi za astashahada, stashahada na shahada ya kwanza.

No comments:

Post a Comment