KUKOSEKANA kwa maeneo yaliyopimwa kwaajili ya wafugaji imeelezwa ndio sababu
inayochangia migogoro sugu ya wakulima na wafugaji nchini.
Hayo yameelezwa leo bungeni mjini Dodoma na mbunge wa Meatu
kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo chadema Mheshimiwa Meshack Opulutwa
wakati akichangia bajeti ya wizara ya mifugo na Uvuvi.
Amesema , mifugo inachangia pato kubwa la nchi na baadhi ya mikoa
inayotegemea mifugo ambapo alitoalea mfano wa mkoa wa Simiyu amabo umepata
shilingi bilioni 27 mwaka 2013/2014 kutokana na mifugo ikiwa na watu
milioni 1.5 na ng’ombe milioni 2 huku ikipata maziwa lita milioni 21 kwa mwaka
No comments:
Post a Comment