KATIBU wa mfuko wa
jimbo la kilosa kati Mtila Mbaruku amewataka viongozi wa vijiji vilivyoko kata
ya kidete wilayani Kilosa kusimamia kikamilifu mradi wa ukarabati wa visima vya
maji kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa vijiji hivyo.
Akizungumza may 23 mwaka huu Mtila
Mbaruku ambaye pia ni Afisa wilaya ya Kilosa katika ziara ya ukaguzi wa miradi
ya maendeleo katika kata ya kidete na Lumuma iliyojumuisha ukarabati wa visima
vine vya maji amesema kuwa wananchi wanapaswa kufahamu kuwa visima hivyo vya
wananchi wa vijiji hivyo.
Amesema kuwa visima hivyo
vinakarabatiwa kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo baada ya mbunge wa jimbo la
Kilosa kati Mustapha Haidi Mkulo kuona umuhimu kuwapelekea maji wananchi wa
vijiji hivyo kutokana na shida ya maji wanayoipata.
Amesema kuwa Mkulo amenunua vifaa
vya kukarabati visima vya vijiji vya kitati , mwasa, manolowe na mzaganza
ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi kwa wananchi wa kata ya Kidete wakati
wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010.
Hata hivyo Mtila amewataka wananchi
kuhudhuria kwenye mikutano ya kijiji ili kuwasilisha na kuibua hoja za miradi
ya maendeleo na kupata majibu sahihi kutoka kwa viongozi wao na siyo
kutoa lawama zisizo kuwa na msingi kwa viongozi wa ngazi za juu.
No comments:
Post a Comment