Saturday, May 24, 2014

WANANCHI washajiishwa kutoa ushirikiano kwa wataalamu ili kujiletea maendeleo



JUKUMU la kuleta maendeleo katika jamii halina budi mwenda sanjari na wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalamu,Imeelezwa.

Mtaalamu wa lishe toka Chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine cha mjini Morogoro Bwana Mnyika Stewart ameeleza hayo mapema jana katika mahojiano maalum na Mbiu ya maendeleo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Amesema  wananchi wengi hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa wataalamu hasa katika  masuala ya ufikishwaji wa taaluma na teknolojia mbalimbali za afya  hali inayopunguza  ari na moyo kwa baadhi ya wataalamu.

Kutokana na hali hiyo ametoa wito kwa maafisa maendeleo ya jamiii na uongozi wa kata na wilayani kutoa elimu ya mara kwa mara ili kuleta mabadiliko chanya ndani ya jamii.

No comments:

Post a Comment