Saturday, May 24, 2014

JUMLA ya mbwa 70 wapatiwa chanjo wilayani Kilosa.



JUMLA  ya mbwa 70 wamepatiwa chanjo katika  tarafa ya Kilosa mjini,wilayani Kilosa, mkoa wa Morogor oili kuwakinga na ugonjwa wa kichaa cha mbwa
Akizungumza na mbiu  ya maendeleo mapema leo mjini Kilosa, Afisa wa mifugo wilaya  

 Dokta David Shemweta  amesema zoezi hilo limeusisha kata nne za tarafa ya Kilosa mjini ambapo kutokana na idadi hiyo ndogo ya mbwa waliopelekwa na wamiliki wao kupatiwa chanjo hiyo zoezi ilo litafanyika tena  wiki ijao ya mei 31 mwaka huu ili kuwapa nafasi ambao mbwa wao hawajapatiwa chanjo .

Ameongeza  zoezi hilo la chanjo cha kichaa cha mbwa hufanyika kila mwaka mara moja ikiwa ni pamoja na kutoa  dawa ya minyoo ambayo hutolewa kila baada ya miezi mitatu ambapo amesema kuwa iwapo mbwa asipopatiwa chanjo ya kichaa cha mbwa mara ang’atapo mtu hupata ugonjwa wa kichaa cha mbwa .

No comments:

Post a Comment