CHANGAMOTO
imetolewa kwa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuhakikisha kuwa wananchi wanapatiwa elimu ya kutosha kuhusu kuongezwa kwa alama za ufaulu kupitia
vipindi vya elimu kwea umma kwa njia ya redio na runinga.
Wakiongea na Mbiu ya maendeleo
jijini Dar es salaam jana katika banda la Baraza la mitihani la Taifa( NECTA) kweny e kilele cha maonesho ya vyuo vikuu,
badhi ya wananchi wamesema kuwa, kushambuliwa sana kwa wizara ya elimu kuhusu
alama za ufaulu ni kutokana na kitengo cha elimu kwa umma kutokuwa na vipindi ,
hivyo wakati umefika kwa wizara husika kuondoa sintofahamu hiyo ndani ya jamii.
Wamesema jamii hasa wadau wa elimu
wamekuwa na mtazamo hasi kuhusu kuongezwa alama na madaraja ya ufaulu kutokana
na kukosa ufafanuzi toka mamlaka husika.
Asilimia kubwa ya wananchi waliotembelea
maonesho hayo walikuwa wananchi wa liomaliza kidato cha nne na sita ili kupata
ushauri na ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali yanyohusu vyuo vya ndani na nje ya
nchi.
No comments:
Post a Comment