Monday, May 26, 2014

Mustapha Mkulo atangaza kustahafu siasa



MBUNGE wa Jimbo la Kilosa Mustapha Haidi Mkulo ameamua kutoa dukuduku lake la muda mrefu kabla ajafa kuwa hakuusika wala hakushiriki katika  mchakato wa kuuza kiwanja no. 10 cha shirika Hodhi la mali za serikali (CHC) wakati alipokuwa waziri wa fedha nchini.

Mkulo amesema hayo hivi karibuni wakati  akizungumza na wazee wa jimbo lake juu ya tuhuma iliyomkabiri ya uuzwaji wa kiwanja hicho kilichotajwa  kuwa kiliuzwa kinyume cha utaratibu kwenye ripoti ya mwaka 2010/2011 na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) .

Mkulo amesema kuwa tangu apate tuhuma hiyo hakuwai kupata nafasi yoyote kwenye ngazi za serikali ili aweze kutetea juu ya tuhuma hiyo na kwamba ameamua kuliweka wazi kwa wazee wake wa baraza katika jimbo la Kilosa kuwa hakuhusika kwenye mchakato mzima wa uuzwaji wa kiwanja hicho.

Amesema kuwa si yeye tu hakuhusika hata wizara yake ya fedha pia haikuwa ikihusika na kuongeza kuwa wakati kiwanja hicho kinauzwa yeye alikuwa nchini  Marekani kwa majukumu mengine ya kitaifa.
Sambamba na hayoMbunge huyo amesisitiza kutangaza kuwa anastahafu siasa na hatakuwa tayari kugombea tena ubunge ifikapo 2015 ni katika kutimiza azma ya kuwa mbunge kwa vipindi viwili bali sasa ataendelea kuwa mwanachama wa kawaida.



No comments:

Post a Comment