Monday, May 26, 2014

Kikao cha bunge la bajeti chaendelea mjini Dodoma



BUNGE  limeendelea kujadili makadirio ya bajeti ya wizara ya uchukuzi mjini Dodoma kwa baadhi  ya wabunge kuchangia mjadala wa wizara hiyo.
Awali akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani Mheshimiwa Moses Machali ameishutumu serikali kwa ufisadi wa matumizi mabaya ya fedha   zinazotolewa na serikali kwa miradi  mbalimbali.
 Aidha amesema kuna matumizi mabaya ya madaraka serikalini,yanayo sababisha  dhuluma na ufisadi, akitolea mfano manyanyaso ya faini wanazotozwa waendesha pikipiki nchini maarufu kama bodaboda yanayofanywa na  mamlaka husika.

Kwa upande wake mbunge wa bariadi mashariki mheshimiwa Andrew Chenge ameishauri serikali kupitia wizara ya Uchukuzi isiitegemee benki ya Dunia katika kutekeleza majukumu yake hasa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali pia ameiomba serikali iachane na visingizio vya muda mrefu kwa wizara hiyo juu ya upembuzi yakinifu na usanifu kwa miradi hiyo.

Ushauri mwingine umetolewa na mheshimiwa James Mbatia ambapo yeye kwa upande wake amesema Serikali ifanye maamuzi magumu katika kutekeleza majukumu yake kuliko kubaki na hali ya kushuka na kupanda katika miradi yake.

No comments:

Post a Comment