JUMLA
ya vyandarua 260 vyenye thamani ya shilingi milioni mbili na themanini elfu
vimetolewa na shirika la compassion Tanzania kituo cha 552 kwa kushirikiana na
kanisa la Moravian usharika wa Morogoro mjini.
Akizunguza
katika hafla hiyo ya kutoa vyandarua hivyo kwa watoto wanaoishi katika
mazingira hatarishi na yatima,mchungaji wa kanisa hilo bwana Lawi Mwankuga
ameitaka jamii kuvitumia vyandarua hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuacha
kuvitumia kwa ajili ya kufugia kuku na mambo mengine ambayo yanarudisha
nyuma juhudi za kupambana na ugonjwa wa malaria
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa compassion Tanzania wa kituo cha 552 bi Josephine
Donald amesema wafadhili wa shirika hilo wameamua kujinyima kwa kidogo walichonacho
ili kuwasaidia watoto wa kitanzania waishi katika mazingira yaliyobora huku
bwana Bonifani Nyangala akisema kuwa msaada huo umetolewa wakati muafaka ambapo
taifa limekumbwa na ugonjwa wa Dengue.
Shirika la
compassion Tanzania lilianzishwa mwaka 2004 ambapo kwa sasa limetimiza miaka
kumi na tatu tangu kuanzishwa kwake limekua likitoa huduma mbalimbali kwa
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ikiwemo elimu,afya pamoja na
huduma za kiroho
No comments:
Post a Comment