JUMLA ya shilingi milioni mbili laki tano na elfu
sabini na tano zimetumika katika ujenzi wa vyumba vitano vya nyumba ya mwalimu
katika shule ya sekondari ya Iwemba iliyopo katika kata ya kidodi wilayani
Kilosa mkoani Morogoro .
Hayo yameelezwa na afisa mtendaji wa
kijiji cha Iwemba bwana Jonasi Adamu Mathias wakati akitoa taarifa ya ukarabati
wa mradi huo kwa wajumbe wa mfuko wa jimbo la kilosa hivi karibuni .
Bwana Mathias amesema kuwa
kati ya fedha hizo zilizotoka katika mfuko wa jimbo la Kilosa ni shilingi
milioni mbili laki sita na elfu themanini na nane na nyingine shilingi laki
tatu na elfu tisini zimetolewa na wananchi ambapo fedha hizo zimetumika katika
upauwaji ,kuweka dali ,umeme ,lipu pamoja flow katika nyumba hiyo .
Amesema kuwa mradi huo wa nyumba
umeanza kutekelezwa tangu mwezi wa nne mwaka huu ambapo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa
sita kwasasa ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 85 .
No comments:
Post a Comment