MAONESHO ya siku mbili ya Elimu ya msingi ya
Mnazi mkinda yaliyoandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya
Ilala kwa kushirikiana na Taasisi ya Insider Tanzania ya
meanza leo
katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam, na yanarajia kumalizika
hapo kesho.
Akiongea na
mbiu ya maendeleo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dra es salaam mapema
leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Insider Tanzania Bwana Aaron Kinega ,
amesema kuwa Falsafa ya “Mnazi Mkinda” ilianzishwa miaka mitatu iliyopita ukiwa na lengo na kuongeza ufaulu na ubunifu
kupitia elimu nya darsani na uibuaji wa vipaji vya wanafunzi kupitia michezo
katika manispaa ya Ilala
Falsafa
hiyo inatimiza malengo ya matokeo makubwa sasa yaani BRN kama ilivyozoeleka
Katika
falsafa hiyo mwanafunzi anatakiwa atoke kwenye kkk kuelekea KKK yaani kutoka
kusoma,kuandika na kuhesabu (kkk) akomae zaidi na kwenda Kujitambua , kujiamini
na kujitegemea.(KKK)
Maana ya
mnazi mkinda ni mnazi mchanga yaani kumlea mwananfunzi mpaka afikie hatua ya
kujitegemea
|
No comments:
Post a Comment