Tuesday, May 27, 2014

MKUU wa wilaya amtaka Mwenyekiti wa miwa kuendelea na madaraka yake



MKUU wa wilaya ya Kilosa,mkoani Morogoro  Elias Tarimo amemtaka mwenyekiti wa chama cha wakulima wa miwa MSINDAZI CANE GROWERS ASSOCIATION (MCGA) kilichopo Ruaha wilayani humo,Bwana  Ayubu  Mora kuendelea na madaraka mpaka muda wake utakapo kwisha ili atatuwe changamoto zinazokikabili chama hicho.
Tarimo ametoa kauli hiyo hivi karibuni kwenye mkutano mkuu wa wakulima na viongozi wa chama hicho uliohusu kusomewa taarifa ya ukaguzi na mapato na matumizi ya chama mwaka 2009 hadi 2014 .

Tarimo amemtaka kiongozi huyo kuendelea na madaraka kutokana na mgogoro ulioko kati ya wanachama na viongozi wa chama hicho juu ya deni la jumla ya zaidi ya shilingi milioni mia moja arobaini zinazodaiwa baada ya kukopa kutoka kwa wanachama , wahisani, na Bank ya CRDB kwa ajili ya kununua gari la kupakia miwa (Cane loader).

Awali mwenyekiti Ayubu Mora aliwataarifu wanachama kuwa baada ya kusomewa taarifa ya mapato na matumizi atajiudhuru na kujiondoa katika nafasi hiyo ili uchaguzi wa muda ufanyike ,ndipo wakulima waliibua hoja mbalimbali juu ya uhai wa chama na kusema kuwa endapo mwenyekiti huyo atajiudhuru viongozi wengine na wanachama  wataondoka katika chama hicho hivyo kupoteza uhai wa chama .







   
     

No comments:

Post a Comment