Tuesday, May 27, 2014

KAMATI ya ardhi ya wilaya ya Kilosa yakabidhi serikali ya kijiji hekari 14666 kwaajili ya kuwagawia wananchi wa kijiji cha Mbigili



KAMATI ya Ardhi ya kugawa mashamba Wilayani Kilosa,mkoani Morogoro  imekabidhi mashamba kwa serikali ya kijiji cha Mbigili kilichopo kata ya Magole wilayani humu zaidi ya hekari 1466 kwa ajili ya kuwagawia wananchi wa kijij hicho kwa ajili yashughuli za  kilimo.

Akizungumza na mwandishi wetu  mapema leo Afisa Ardhi na mali asili wilaya Bwana Ibrahimu Ndembo amesema kuwa mashamba hayo ambayo yamekabidhiwa kwa serikali ya kijiji yalifutwa na Rais Jakaya Kikwete  umiliki kutoka katika kampuni ya MES ESTATE  LIMITED  mwaka 2000.

Ndembo amesema kuwa baada ya Rais Kikwete kufuta umiliki wa mashamba hayo no. 28 ,29 na32 kutoka kwa mmiliki wa kampuni hiyo kutoka Dar es salam kikao  cha kugawa Ardhi cha wilaya kiliamua mashamba hayo yagawiwe kwa wananchi ili kuondoa mgogoro wa muda mrefu kati ya wananchi na mmiliki wa kampuni hiyo ambaye alileta  sintofahamu kati yake na wanakijiji ikiwa ni pamoja na kuwapeleka mahakamani baadhi yao kwakila mwananchi aliyekuwa akifanya za kilimo katika  shamba hilo.

Amesema kuwa baada ya kamati hiyo kuwakabidhi hekari hizo za mashamba serikali ya kijiji hicho cha Mbigili imewataka kuhakikisha mpaka kufikia  tarehe moja mwezi wa sita mwaka huu wahakikishe wameshawagawia wananchi maeneo ya kilimo na ikipendekeza kuwa kitongoji cha  Mateteni kipewe kipaumbele kwani akina eneo kwa ajili ya kilimo .


No comments:

Post a Comment