WAZIRI
wa ardhi , nyumba na maendeleo ya makazi jana ametembele wilaya ya Mvomero,Mkoani
Morogoro kwa lengo la kukagua mipaka katika vijiji vilivyopo wilayani humo.
Katika
ziara hiyo Waziri Tibaijuka amezungumza na wananchi wa kijiji cha Lukenge na
kusema kuwa suala la kusimamia ardhi linahitaji umakini ili kuepuka migogoro
inayotokana na ardhi.
Prof
Tibaijuka amesema kuwa vijiji 31 vimeandaliwa kwa ajili ya kupimwa
na vingine nane vinahakikiwa huku akiwaagiza wakulima na wafugaji
kundelea kuishi kwa amani kwani mfugaji ana haki ya kufuga na mkulima anayo
haki ya kulima.
Awali
akisoma Risala kwa niaba ya wanakijiji wa Lukenge Afisa Mtendaji wa kijiji
hicho bwana Ally Kingu amesema wanaishukuru serikali kwa kukarabati jengo la
Masjala ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni sita laki nane na
ishirini elfu ambapo waziri Tibaijuka amelifungua rasmi wakati wa ziara yake.
Kijiji
cha Lukenge kina jumla ya Ng’ombe elfu nne na mbuzi zaidi ya elfu tatu ambapo
katika ziara hiyo pia waziri Tibaijuka alitembelea shamba la mfano la ukulima
wa nyasi kwa ajili ya malisho.
No comments:
Post a Comment