BODI
ya usajili wa makandarasi inayosimamia
shughuli zote za ukandarasi nchini, inatarajiwa kufanya mkutano wa siku mbili
kujadili ufanisi wa Makandarasi katika majukumu yao pamoja na kuangalia mamlaka
zinazosimamia shughuli za makandarasi.
Akizungumza na waandishi wa habari,jijini
Dar es salaam,mwenyekiti wa bodi ya makandarasi,bwana Boniface Muhegi, amesema
mkutano huo pia utatathmini changamoto zinazowakabili makandarasi na namna ya
kuzitatua pamoja na kuboresha utendaji wao, ukiambatana na maonesho ya
makandarasi na vifaa vya ujenzi.
|
Sambamba na hilo amesema katika mkutano
huo, wahandisi ambao hufanyakazi na makandarasi wataapishwa kudumisha maadili
ikiwemo kutoshiriki vitendo vya rushwa pamoja na kusimamia kazi zao kwa
weledi ili kuwaimarisha kazi zao.
|
No comments:
Post a Comment