Wednesday, May 28, 2014

MTOTO aliyeishi kwenye boksi kwa miaka mitatu ahamishiwa Muhimbili kwa matibabu zaidi

MTOTO aliyeishi  kwenye boksi kwa mudamrefu ahamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi kutokana  na uwezo mdogo wa hospitali ya Morogoro wa  vifaa .

Akiongea na Mbiu ya Maendeleo mjini   Morogoro mapema jana ,mganga mkuu wa hospitali hiyo Daktari Hores Msacky  amesema  tulimpokea mtoto huyo  akiwa katika hali ya uchafu usio wa kawaida na tuliamua kumfanyia vipimo vya awali pamoja na picha za X ray, ambaapo imegundulika kuwa mifupa yake  inaonekana imevunjika ingawa hawajajua nini kimemvunja.



. Hata hivyo Msaky alisema kuwa hospitali hiyo haina vifaa vingi vya kupimia mifupa, hivyo mtoto huyo atapelekwa  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.  

DSC01720nesi 1
Muuguzi katika Wodi ya watoto hospitali ya rufaa ya Morogoro akimuhudumia mtoto Nasra Said mara baada ya kufikishwa hopsitalini hapo kupatiwa matibabu.

Baba mzazi wa mtoto huyo alisema yeye ana mke na watato wengine wa ndoa na kwamba hakuwahi kumwambia mkewe kama ana mtoto wa nje hivyo ilikuwa vigumu kumchukua mtoto huyo na ndipo alipomkabidhi mama mkubwa wa mtoto huyo.

mtoto 2
Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa.
Baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi mwanamke huyo alikiri kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa na umri wa miezi tisa na kwamba hatua hiyo ilikuja baada ya mama yake, kufariki dunia mwaka 2010.
Hata hivyo majirani hao walidai wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikina kutokana na kwamba mama huyo anaakili timamu na analea watoto wake vema tofauti na mtoto huyo.

No comments:

Post a Comment