IMEELEZWA kuwa mwamko mdogo katika uchangiaji damu kwa
mamlaka zinazohusika na ukusanyaji wa damu salama nchini ndio chanzo kikubwa
cha ukosefu wa damu katika benki za damu kwenye hospitali mbalimbali
nchini,hali inayochangia vifo vingi vingi vya kinamama wakati wa kujifungua.
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na mkurugenzi wa tiba ,wa
wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk MAGRETH MHANDO, katika hotuba iliyosomwa
kwa niaba yake na Dk.PAULO MHAME wakati wa uzinduzi wa warsha ya siku moja ya
viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini pamoja na maofisa kutoka
serikalini,waandishi wa habari na wadau wa damu salama.
Amesema hali hiyo inatokana na wananchi kutopatiwa elimu ya
kutosha juu ya uchangiaji wa damu kwa kukidhi mahitaji yanayosababishwa na
matukio mbalimbali ndani ya jamii huku baadhi ya wanajamii wakiamini kuwa kwa
kufanya hivyo kuna kitu wanachopoteza.
No comments:
Post a Comment