WITO umetolewa kwa Taasisi,mashirika na wafanya biashara mbalimbali wilayani Kilosa
,mkoani Morogoro kujitokeza kuchangia mifuko ya maendeleo ikiwemo hasa sekta ya
elimu.
Akiongea na mbiu ya maendeleo ofisini kwake mapema leo
Afisa Mtendaji kata ya Kasiki iliyopo
mamlaka ya mji mdogo Kilosa Ferdinand Weteka amesema ni vizuri Taasisi na
mashirika kama TANESCO na CRDB kuiga
mfano wa NMB ambao wamekuwa mbele kuchangia katika elimu
Amesema Bank ya NMB imechangia
zaidi ya madawati themanini yenye thamani ya shilingi milioni tano kwenye shule
ya sekondari Dendego iliyopo kata ya Kasiki,wilayani Kilosa ambayo
tayari yapo kwenye mchakato wa kukamilika .
No comments:
Post a Comment