AFISA takwimu wa wilaya ya Kilosa Mtila Mbaruku ameuagiza
uongozi wa kijiji cha kivungu wilayani Kilosa kukarabati upya ofisi ya kijiji
hicho .
Mtila ameyasema hayo ivyi karibuni
wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Jimbo
la Mikumi na kusema kuwa jengo hilo la ofisi ya kijiji alijakidhi viwango kwani
limepauliwa kwa mbao chakavu lakini pia milango inayotumika aina
kiwango .
Aidha ameongeza kuwa Wilaya ya
Kilosa ina takribani vijiji 118 ambavyo vinahitaji pesa kwa ajili ya kuanzisha
na kurabati miradi mbalimbali lakini kijiji cha kivungu kimebahatika kupata
fedha hizo lakini wanavitumia kinyume na malengo .
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji
cha kivungu Antony Adrian wakati akijibu taarifa ya jengo kuwa chini ya kiwango
amekiri mapungufu yaliyopo na kuahidi kuwa atahakikisha watarekebisha
mapungufu yaliyopo katika jengo hilo.
No comments:
Post a Comment